SALAMU ZA SHEREHE YA KUMBUKIZI YA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI KUTOKA MOBILE FACILITATION TEAM (MOFATE).

SALAMU ZA SHEREHE YA KUMBUKIZI YA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI KUTOKA MOBILE FACILITATION TEAM (MOFATE).

○ Leo ni tarehe 8th March 2024, ni siku njema kama kumbukizi ya mwanamke duniani! Ni siku inayotawaliwa na furaha, amani na upendo katika mioyo ya wanawake wote duniani! Kumbukumbi hii inabeba hisia njema sana zenye furaha ya machozi kutokana na mambo mbalimbali ya kitamadunini ambayo wanawake wamepitia katika karne kadhaa hapo nyuma hasa katika utamaduni wa ushirikishwaji katika masuala mablimbali na maamzi katika tambuzi ya yapi ambayo wao kama wanawake wanaweza kuwa na mchango katika nyanja za kijamii, kiuchumi, kimwili na kifikra!. Walipitia mazingira mengi ambayo hayakuwa na kuwapa mianya ya kufanya bidii zenye matokeo chanya wazi kwa vizazi! Kupitia siku yenu muhimu wanawake ninapenda sana kushare nanyi machache ambayo huenda ni sehemu ya kuwakumbusha tu ili yaendelee kujenga furaha na amani ya familia zetu badala ya kutubadilisha kabisa na kutupeleka katika mazingira ambayo hayatakuwa na tija kwa familia zetu!

♡ Mwanamke anavalishwa ushujaa siku hii ya leo tungependa kumuona kwamba mapambano yake haya mtenganishi yeye na familia yake muda wowote, kwasababu kiafya maelezo yake ni muhimu sana!

♡ Mwanamke anavalishwa ushujaa siku hii ya leo tungependa kumuona kwamba mapambano yake hayaathiri mahusiano yake na mume wake hasa kutokana na ukubwa na mafanikio yake kiuchumi.

♡ Mwanamke tunayemvalisha leo hii ushujaa tungependa kumwona kwamba mapambano yake hayamtenganishi yeye na heshima za kiutamaduni kati yake na familia, ndugu na rafiki zake ambao kwa nyakati tofauti zinamhitaji.

♡ Mwanamke tunayemvalisha leo hii ushujaa tungependa kumwona kwamba mapambano yake hayamtenganishi yeye na unyenyekevu kwa Mungu na familia yake hasa mumewe wakati wa maamzi ya utekelezaji wa mipango mbalimbali.

♡ Mwanamke tunayemvalisha leo hii ushujaa tungependa kumwona kwamba mapambo yake yaende sambamba na maamzi sahihi ya mahusiano yake hasa umri, siyo uchumi uwe wa kuwa na mahusiano na vijana wadogo kwani hali hii ni kudhalilisha ushujaa tunaokuvalisha!

♡ Mwanamke tunayemvalisha ushujaa leo hii tungependa kumwona kwamba katika kila mapambo yake yakutafuta ushujaa huu hayaathiri eneo la malezi kwa watoto badala ya kuwatelekeza siku nzima au nyakati mbalimbali.

♡ Mwanamke tunayemvalisha ushujaa leo hii tungependa kumwona  katika kila maamzi yake hasa ya uchumi hajiingizi katika mikopo mbalimbali isiyoshirikishi na mwishowe kuwa mtumwa wa rushwa ya mwili wake bali, ile inayoweza kulinda afya yake mwenyewe!

♡ Mwanamke tunayemvalisha ushujaa leo hii tungependa kumwona kwamba katika kila mapambao yake hahusiki na utoaji wa mimba haramu kwasababu bado tunahitaji tuendelee kuona wanawake wengine wengi wanazaliwa ili kuendelea kuwa na mashujaa.
♡ Mwanamke tunayemvalisha ushujaa leo hii hasa katika nyanja ya uongozi tunapenda kumwona kwamba katika mapambano yake ya kila siku anatumia nafasi yake kuwahurunia wanateseka na changamoto za maisha, anasuluhisha migogoro zaidi kuliko kuwa chanzo, anabadilisha mawazo ya watu kuwa maisha na kuwatia nguvu wengine kufika nafasi yake badala ya kuwafitini zaidi.

♡ Mwanamke tunayemvalisha ushujaa leo hii katika nyanja mbalimbali hasa katika eneo uchumi, hatumii katika harakati za kujilimbikizia kiburi, majivuno na dharau kwa watu wake wa  muhimu sana katika maisha yake kwasababu kufanya hivyo kunawafanya wengine hao kujinyonga ama kupoteza maisha katika njia mbalimbali kutokana misongo ya mawazo.

♧ Baada ya haya machache nichukue nafasi hii kuwapongeza sana wanawake wote duniani na kwa nafasi ya pekee Nchini Tanzania ambao leo hii wamekuwa ni jicho la wengi kama mfano kutokana mafanikio yao! Najua kupitia wao leo hii wengine tumepapata nguvu, makongamano yetu yamekuwa na nguvu kubwa ushawishi mkubwa sana kutokana na wao kuonekana!
☆ Hongera sana Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA leo umewaheshimisha wanawake wote hasa Taifa la Tanzania. Mobile Facilitation Team tunawatakia kila kheri wanawake wote duniani kwa kumbukizi ya siku yenu, sisi wanaume pia tunafurahi sana mafanikio yenu kwasababu mlipo tupo, mafanikio yenu sisi pia ni sabababu pia!

Mosses Evaristo
President- Mofate
08 March 2024
info@mofate.com
www.mofate.com

Share your love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *